Pages

Ads 468x60px

Featured Posts

Wednesday, June 19, 2013

MRISHO MPOTO NA MJOMBA BAND KUHAMASISHA KAMPENI YA KUNAWA MIKONO KWA SABUNI NA UJENZI WA VYOO

IMG_1058  
Msanii wa kughani na kuimba nyimbo za asili Mrisho Mpoto ambaye pia ni Mkurugenzi wa ‘Mjomba Band’ akizungumza na Mhariri wa Mo Blog Lemmy Hipolite (kushoto) kuhusiana na kampeni ya kunawa mikono kwa sabuni na ujenzi wa vyoo bora ili kuepukana na maradhi yanayosababishwa na uchafu. Kampeni hiyo itafanyika katika mikoa mitano hapa nchini ikianzia na Dodoma, Mara, Njombe. Rukwa na Tanga.
Na Mo Blog
Mwanamuziki na mghani maarufu wa nyimbo za asili ya nyumbani Mrisho Mpoto amewataka wasanii na wanamuziki wote nchini Tanzania kuwa kitu kimoja kwa kujenga ushirikiano na muungano ili kuweza kuufikisha muziki wa hapa nyumbani katika malengo ya kimataifa.
Akizungumza na Mtandao Maarufu wa Habari jijini Dar es Salaam, Msanii huyo Mrisho Mpoto maarufu kama ‘Mjomba’ amesema katika kujulikana kwenye michezo kama inayofanyika kwa sasa, vikundi vya uhamasishaji vinavyotumia sanaa ya asili ni muhimu kutumika ili kuweza kukuza lugha pamoja na utamaduni wa nyumbani.
Amesema ili kufanikisha usafi wa mazingira ikiwemo siku ya kimataifa ya kunawa mikono ni muhimu jamii ya watanzania kuzingatia usafi ili kuepukana na magonjwa ya kuambukiza yanayotokana na uchafu unaoambukiza maradhi yanayotokana na uchafu.
Aidha amesisitiza jamii kujenga utamaduni wa kujenga na kutumia vyoo bora na kuboresha mzingira kwa ujumla ili kuhakikisha elimu hiyo inawafikia walengwa kwa kubadili tabia na njia mbadala za mawasiliano kuhusu elimu hiyo.
Amesema mwaka 2010 aslimia 9 tu ya wananchi waishio vijijini na asilimia 22 ya wananchi waishio mijini waliweza kupata huduma bora za usafi wa mazingira.
Katika kampeni hiyo Mrisho Mpoto na kundi lake la Mjomba Band wataanzia mikoa ya Dodoma, Mara, Njombe, Rukwa na Tanga kabla ya kuendelea mikoa mingine ambayo kwa pamoja na watashirikianana na Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii.

Tuesday, June 18, 2013

MCHEZAJI WA TANZANIA APATA ULAJI YEMEN

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetoa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa mchezaji Mtanzania Gossage Mtumwa ili aweze kucheza mpira nchini Yemen. 
Mtumwa ambaye anatoka katika kituo cha kukuza na kuendeleza vipaji cha Rollingstone cha Arusha aliombewa hati hiyo na Chama cha Mpira wa Miguu cha Yemen (YFA) kwa ajili ya kucheza nchini humo. 
TFF inamtakia kila la kheri Mtumwa katika safari yake ya Yemen, na ni matarajio yetu kuwa atakuwa balozi mzuri wa Tanzania nchini humo ili wachezaji wengine wa Tanzania nao wapate fursa ya kucheza mpira wa miguu nchini Yemen.

HABARI NJEMA KWA WACHEZAJI WA KITANZANIA ULAJI HUOOOO

Klabu ya Thai Port Football ya Thailand inatafuta wachezaji nchini Tanzania kwa ajili ya kucheza mpira wa miguu nchini humo na katika nchi nyingine barani Ulaya. 
Kupitia kwa wakala wake, klabu hiyo imetuma taarifa kupitia Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ikitaka wachezaji wenye umri kuanzia miaka 15 hadi 28 kwa ajili ya kuwafanyia majaribio ambapo watakaofuzu watacheza nchini humo na katika klabu nyingine za Ulaya ambazo wana ushirikiano nazo. 
Wachezaji wenye nia ya kufanya majaribio wanatakiwa kutuma taarifa za wasifu wao (CV) kwa klabu hiyo kwa njia ya emaili, wawe na pasi ya kusafiria pamoja na pasi ya mchezaji (player passport). 
Wakala atapitia vitu hivyo, na kwa wachezaji atakaowahitaji atawatumia tiketi za ndege na viza kwa ajili ya kwenda kufanya majaribio nchini humo, na watakaofanikiwa kabla ya kusaini nao mikataba watawasiliana na klabu zao nchini (kwa wale wenye klabu).

IDDI AZZANM, HALIMA MDEE WAJIFUA TAYARI KUWAKABILI WOLPER, MDEE KATIKA TAMASHA LA MATUMAINI

Halima Mdee na Idd Azan wakijifua mkoani Dodoma.
Mazoezi yakiwa yamepamba moto.
Video
Mdee akijiimarisha kwa ajili ya kumkabili Wolper.
Mbunge wa Kawe, Halima Mdee na Idd Azan ambaye ni Mbunge wa Kinondoni, wameanza kujichua kwa ajili ya mapambano yao ya ndondi katika Tamasha la Matumaini 2013 litakalofanyika Julai 7 katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Halima Mdee atazipiga na Jacqueline Wolper wakati Idd Azan akionyeshana ubabe na Jacob Steven 'JB'
(Picha na Luqman Maloto /GPL, DODOMA)
PICHA NA VIDEO:

RWIZA KUHUDHURIA SEMINA YA MAKAMISHNA WA SOKA ILIYOANDALIWA NA CAF

Kamishna Alfred Kishongole Rwiza ameteuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kuhudhuria semina ya makamishna itakayofanyika kuanzia Julai 6-7 mwaka huu katika makao makuu ya shirikisho hilo jijini Cairo, Misri.

Semina hiyo inashirikisha baadhi ya makamishna wa CAF walioko kwenye orodha ya makamishna ya shirikisho hilo kwa mwaka 2012-2014.

Rwiza ni mmoja wa makamishna wa CAF kutoka Tanzania, na mechi ya mwisho kusimamia ilikuwa ya Kombe la Shirikisho iliyochezwa Mei mwaka huu nchini  Msumbiji.

CAF tayari imeshamtumia tiketi Rwiza, na anatarajia kuondoka nchini Julai 4 mwaka huu kwenda Cairo kwa ndege ya EgyptAir.

WAPONGEZWA KWA KUIUNGA MKONO TAIFA STARS

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linawashukuru washabiki kwa kujitokeza kwa wingi kwenye mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia kati ya Taifa Stars na Ivory Coast (The Elephants) iliyochezwa juzi (Jumapili) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mwitikio wa washabiki katika mechi hiyo ilikuwa ni moja ya chachu ya kiwango kilichoonyeshwa na Taifa Stars, kwani walishangilia mwanzo hadi mwisho licha ya kupoteza kwa mabao 4-2. 
Ni matarajio utakuwepo mwitikio kama huo huo katika mechi ijayo ya Taifa Stars ya michuano ya Afrika kwa Wachezaji wa Ligi za Nyumbani (CHAN) dhidi ya Uganda (The Cranes) itakayochezwa Dar es Salaam kati ya Julai 12-14 mwaka huu. Stars itaingia tena kambini Julai 4 mwaka huu kujiandaa kwa mechi hiyo.

KOZI YA MAKOCHA WA SOKA NGAZI YA PILI KUFUNGWA JUMANNE IJAYO

 Kocha mkuu wa Twiga Stars akitoa somo kwa makocha wa kozi ya ngazi ya pili kwa vitendo
 Kocha mkuu wa Twiga Stars, Rogasian Kaijage akitoa somo kwa makocha wanashiriki kozi ya ukocha ngazi ya pili ndani ya darasa kwenye Ukumbi wa Harbours Club, Kurasini.

Baadhi ya makocha wakiwemo wachezaji wa zamani wakifuatilia mafunzo ya ukocha ngazi ya pili.
 
KOZI ya makocha wa ngazi ya pili (Intermediate) inayosimamiwa na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), inatarajiwa kufungwa Jumanne ijayo baada ya kudumu kwa wiki nne.
Kozi hiyo ilianza Juni 3 mwaka huu kwenye Ukumbi wa Harbours Club, uliopo Kurasini chini ya Mkufunzi Rogasin Kaijage, ambaye ni Kocha wa timu ya Taifa ya Wanawake ‘Twiga Stars’ ambapo makocha mbalimbali pamoja na wachezaji wa zamani wamejitokeza kushiriki.
Ofisa Habari wa DRFA, Mohamed Mharizo alisema kozi hiyo imekuwa na mafanikio na wanatarajia makocha walioshiriki katika kozi hiyo watakuwa na mchango mkubwa katika kuendeleza mpira wa miguu katika mkoa wa Dar es Salaan na Taifa kwa ujumla.
“Hadi sasa tunashukuru kuona tunafanikisha kozi hii ambayo wengi wameitikia wito, mwisho wa kozi hii ndio mwanzo wa kozi nyingine.
“Lakini haya ya kozi ya makocha ni moja ya majukumu ya Kamati ya Ufundi ya DRFA yaliyoainishwa katika Katiba, hivyo hili ni moja ya shabaha yetu na mengine mengi mazuri yanafuata,” alisema Mharizo.
 Kozi hiyo ni ya kwanza kuendeshwa na DRFA tangu kuingia madarakani kwa uongozi mpya wa chama hicho Desemba 12, chini ya Mwenyekiti wake Almas Kassongo.

TIKETI ZA ONYESHO LA BIDHAA ZA HARUSI ZAANZA KUUZWA


Monday, June 17, 2013

STARS KAMBINI TENA JULAI KUJIANDAA NA CHAN

Kocha wa Taifa Stars, Kim Poulsen ameiita tena kambini timu hiyo Julai 4 mwaka huu kujiandaa kwa mechi ya kutafuta tiketi ya kucheza Fainali za Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) zitakazofanyika mwakani nchini Afrika Kusini. 
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager inavunja kambi leo (Juni 17 mwaka huu) baada ya mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia, kundi C Kanda ya Africa dhidi ya Ivory Coast iliyochezwa jana (Juni 16 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 
Kim amesema wachezaji watakaoitwa kambin ni wote walioko kwenye timu hivi sasa isipokuwa Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wanaocheza mpira nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) katika klabu ya TP Mazembe Englebert. 
Wachezaji hao ni Juma Kaseja, Aishi Manula, Aggrey Morris, Mwadini Ally, Ally Mustafa, Shomari Kapombe, Kevin Yondani, Erasto Nyoni, Haroub Nadir, Mwinyi Kazimoto, Frank Domayo, Mrisho Ngasa, Khamis Mchana, Amri Kiemba, Salum Abubakar, Simon Msuva, John Bocco, Vicent Barnabas, Mudathiri Yahya, Athuman Idd, Haruni Chanongo na Zahoro Pazi. 
Mechi hiyo namba 37 dhidi ya Uganda (The Cranes) itachezwa jijini Dar es Salaa kati ya Julai 12 na 14 mwaka huu wakati ile ya marudiano itafanyika wiki mbili baadaye katika Uwanja wa Mandela ulioko Namboole nje kidogo ya Jiji la Kampala.

MIL.500 ZAINGIZWA MECHI YA STARS NA IVORY COAST

Mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia, Kundi C, Kanda ya Afrika kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Ivory Coast (The Elephants) iliyochezwa jana (Juni 16 mwaka huu) imeingiza sh. 502,131,000 kutokana na watazamaji 57,203. 
Tiketi za kushuhudia mechi hiyo ziliuzwa kwa sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 15,000, sh. 20,000 na sh. 30,000. 
Mgawanyo wa mapato hayo ulikuwa kama ifuatavyo; asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ni sh. 76,596,254.24 wakati wa gharama za uchapaji tiketi ni sh. 7,809,104. 
Asilimia 15 ya uwanja sh. 62,658,846.26, asilimia 20 ya gharama za mechi sh. 83,545,128.35 na asilimia 5 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) sh. 20,886,282.09. 
Asilimia 60 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) sh. 250,635,385.06 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 12,531,769.25 ambayo ni asilimia 5 kutoka kwenye mgawo wa TFF. 
Mechi iliyopita ya Stars dhidi ya Morocco (Lions of the Atlas) kwenye uwanja huo iliingiza sh. 226,546,000.

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

MISS TEMEKE WAANZA KUJINOA LEO TCC CLUB CHANG'OMBE

VIMWANA 16 wa kanda ya Temeke, wameanza kujinoa leo(Juni 17) kwenye klabu ya TCC Chang'ombe, tayari kwa kinyanga'nyiro kitakochafanyika Julai 5, mwaka huu katika ukumbi huo.
Idadi hiyo ya warembo ni kutoka Kigamboni, Kurasini na Chang'ombe ambao wanawania taji linaloshikiliwa na Miss Tanzania namba tatu, Edda Sylvester ambaye atakuwa mmoja wa wakufunzi katika kambi hiyo, ambayo pia inasimamiwa na Suzy Mwenda na Shadya Mohamed.
Mbali ya hao, pia kutakuwa na jopo na wakufunzi wa dansi, litakaloongozwa na Bokilo na Charles yote katika kuhakikisha shoo ya mwaka huu, itaendana na ubora wa warembo wanaoshiriki shindano hilo, ambapo kwa hakika Redds Miss Tanzania mwaka huu, bila shaka atatokea katika kanda hiyo, yenye historia ya mafanikio.
Temeke, imewahi kutoa warembo kadhaa miaka ya nyuma waliopata mafanikio katika mashindano hayo, mitindo na kazi nyingine hasa kupata uzoefu wa kujiamini katika njanja mbalimbali.
Miongoni mwao ni Miriam Odemba(1997) aliyepata kuiwakilisha Tanzani katika fainali za mitindo zilizofanyika Nice Ufaransa na kupata mkataba wa Elite Model Look, baadaye kufakinikiwa kutwaa nafasi ya pili ya Miss Earth World, zilizofanyika China.
Pia, Temeke ilimtoa Happines Millen Magesse(2001), na kutwaa taji la Miss Tanzania na kwa sasa anang'ara sana katika tasnia ya mitindo katika nchi za Marekani, Afrika Kusini na barani Afrika kwa ujumla. 2003 Temeke ilimtoa Miss Tanzania, Sylvia Bahame na 2006 kuwatoa Jokate Mwegelo na Irene Uwoya.
Jokate alitwaa taji la Miss Temeke mwaka huu na pia kushika nafasi ya pili Miss Tanzania na pia kushinda taji la ubalozi wa Redd's na gazeti la Citizen. Uwoya ambaye alikuwa mshindi wa pili Temeke alishika nafasi ya nne kwenye Miss Tanzania mwaka huo. Genevieve Mpangala mwaka 2010 alitwaa taji la Miss Temeke baadaye kushinda taji la Miss Tanzania.
Nafasi nyingine za juu zilizowahi kutwaliwa na warembo kutoka Temeke ni pamoja na Irene Kiwia, mshindi wa nne Miss Tanzania mwaka 2000, Regina Mosha mshindi wa nne Miss Tanzania mwaka 2002, Cecylia Assey mshindi wa pili Miss Tanzania 2004, Queen David mshindi wa tatu mwaka 2007 na Edda Sylvester mshindi wa tatu Miss Tanzania akiwa anashikilia taji la Redds Miss Temeke.
Shindano hilo, linalotarajiwa kuwa na burudani ya kipekee limedhaminiwa na kinywaji cha Redd's, Dodoma Wine, Jambo Leo, Blogu ya Wananchi (Le Mutuz), Fredito Entertainment, Kitwe General Traders na CXC Africa tours & Safaris.
Warembo wa Redds Miss Temeke 2013
1-Axsaritha Vedastus,2-Belinda Paul,3-Darling Mmary,  4Esther Muswa, 5-Hyness Oscar, 6-Irene Rajab, 7-Jamila Thomas, 8-Latifa Mohamed,9-Margreth Gerald, 19-Margreth Olotu,11-Mey Karume ,12-Mutesi George, 13-Naima Ramadhan, 14-Narietha Boniface, 15-Stella Mngazija               
16-Svtlona Nyameyo                                       

MISS HIGHER LEARNIG TANZANIA KUANZA KUJINOA IJUMAA @GRAND VILLA HOTEL

WAREMBO wanaotarajiwa kushiriki shindano la Miss Higher Learning 2013 wataanza mazoezi  rasmi Ijumaa ya Juni 21, mazoezi yatakayofanyika kwenye hoteli ya Grand Villa iliyopo Kijitonyama, jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Aggy Classic Entertainment inayoandaa shindano hilo Aggness Mathew alisema kwamba warembo hao watanolewa na mrembo aliyepata kutwaa taji la Kanda hiyo mwaka 2010, Blessing Ngowi (pichani).
 Alisema shindano hilo linatarajiwa kufanyika Julai 5 kwenye ukumbi wa Club Sunsiro ulipo Shekilango jijini Dar es Salaam na kushirikisha warembo 24 kutoka vyuo vikuu vyote vya Tanzania ambapo mwaka huu wamedhamiria kumtoa mshindi wa Miss Tanzania.
 Mratibu huyo aliongeza kuwa, maandalizi mengine kwa ajili ya shindano hilo ambalo taji lake linashikiliwa na Virginia Mokiri kutoka UDOM yanaendelea vema huku akiwaomba wadau na makampuni mbalim,bali kujitokeza kudhamini. 

“Mpaka sasa ni wadhamini wakuu wa Miss Tanzania kinywaji cha Redd’s Original ndio wamethibitisha kudhamini, hivyo tunaomba wadhamini wengine kujitokeza kudhamini shindano letu,”alisema

ADAM MALIMA KUBARIKI TAMASHA LA WASANII MASTAA JUNI 29 KIJIJI CHA MWANZEGA

NAIBU Waziri wa Kilimo, Adam Kighoma Malima (pichani) atakuwa mgeni rasmi katika Tamasha la Wasanii Mastaa litakalofanyika Juni 29, mwaka huu kwenye kijiji cha Mwanzega, Mkuranga mkoa wa Pwani. 
Akizungumza na viongozi wa Mtandao wa Wasanii (SHIWATA) mjini Dodoma katika vikao vya Bunge vinavyoendelea, Malima alisema amekubali kuwa mgeni rasmi vile vile tukio hilo linafanyika katika jimbo lake la uchaguzi la Mkuranga. 
Mwenyekiti wa SHIWATA, Caasim Taalib alisema maandalizi ya tamasha hilo yanaendelea vizuri na kuongeza kuwa kutakuwa na matukio ya wanachama kukabidhiwa nyumba zao kwa wale waliomaliza michango yao akiwemo mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars, Jellah Mtagwa atakabidhiwa nyumba yake. 
Alisema Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida ambaye alikuwa mgeni rasmi tamasha lililopita Mei mwaka huu Dar es Salaam na kuahidi kukarabati barabara za kuingia kijiji cha wasanii Mkuranga atakabidhiwaq kadi pia taasisi yake ya ujasiriliamali ambayo itawakopesha wasanii wa SHIWATA sh. Bil. 7 kwa ajili ya kuendeleza wasanii, itaanza kutekeleza mpango huo wa Awamu ya Kwanza siku hiyo. 
Alisema mbunge wa Kinondoni Bw. Idd Azzan naye atakabidhiwa kadi ya kujiunga na SHIWATA ambako pia wabunge mbalimbali wamealikwa kuhudhuria tamasha hilo akiwemo mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu, Mbunge wa Ilala, Mussa Zungu. 
Wabunge wengine wa mkoa wa Dar es Salaam walioalikwa katika tamasha hilo ni John Mnyika wa Ubungo, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee, na Mwenyekiti wa Taifa wa NCCR- Mageuzi , James Mbatia. 
Alisema mtandao wa SHIWATA ambao umekuwa ukiandaa matamasha ya wasanii kila mwezi limepeleka tamasha la Juni kwenda wilaya ya Mkuranga ambako ndiko zinakojengwa nyumba zao katika kijiji cha Mwanzega-Kimbili ambako mpaka sasa watu nane watakabidhiwa nyumba zao. 
Wasanii 400 kutoka vikundi mbalimbali vikiwemo vya mkoa wa Pwani wanatarajiwa kushiriki katika tamasha hilo . 
Wanachama wa SHIWATA nao wanakaribishwa kuhudhuria tamasha hilo.
  

STARS NDIO BASI TENA BRAZIL 2014

NDOTO za Tanzania kushiriki fainali za  Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil mwaka 2014 zilihitimishwa jana baada ya timu ya Taifa kutandikwa mabao 4-2 dhidi ya Ivory Coast katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
.Katika mchezo huo ambao Stars waliuanza vizuri,  Amri Kiemba aliiandikia Stars bao la kwanza katika dakia ya kwanza ya mchezo huo 
baada ya kupokea kazi nzuri ya Mbwana Samatta.
Dakika ya 12 Traore Lacina aliisawazishia Ivory Coast akimalizia krosi ya Yaya Toure, kabla ya Yaya kupachika la pili katika dakika ya 23 
na dakika ya 34 Thomas Ulimwengu alisawazisha.
Ivory Coast iliandika bao la tatu katika dakika ya 42 lililofungwa kwa penati na Yaya baada ya beki wa Stars Erasto Nyoni kumsukuma Gervinho ndani ya boksi na kufanya timu hizo kwenda mapumziko kwa Ivory Coast kuongoza kwa mabao 3-2.
Kipindi cha pili kilianza kwa mashambulizi ya kupokezana huku Stars ikishindwa kuzitumia vema nafasi ilizozipata ndani ya kipindi hiyo na hatimaye dakika ya 90  Wilfred Bonny alihitimisha karamu la mabao kwa Ivory Coast kwa kupachikia la nne.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL, ALIPOFUNGA TAMASHA LA ASILI LA WATU WA MANGAPWANI UNGUJA

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na Mlezi wa Tamasha la asili la Watu wa Mangapwani, Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha hilo, Mwinyi Jamari Ramadhan Nasib, pamoja na baadhi ya viongozi wakati akiwasili kwenye viwanja vya Mangapwani jana Juni 15, 2013 kwa ajili ya kufunga rasmi Tamasha hilo lililoanza Juni 14. Picha zote na OMR
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia bidhaa zinazotengezwa na vikundi vya akina mama wakati alipokuwa akitembelea mabanda ya maonyesho katika Tamasha la Asili la Watu wa Mangapwani, alipofika kufunga rsmo tamasha hilo jana Juni 15, 2013, mjini Munguja


 Katika Tamasha hilo kulikuwa na mashindano ya michezo mbalimbali ya asili, kama Bao la Kete, Kufua Nazi, na kama mchezo huu pichani vijana wakishindana kukwea Minazi, ambapo kwa upande wa michezo Tamasha hilo lilihitimishwa kwa mchezo wa fainali ya Soka

 Baadhi ya washiriki wa mchezo wa kufua Nazi, wakichuana kufua Nazi hizo ambapo kila mmoja alitengewa jumla ya Nazi 20, na mchezaji wa kwanza (kushoto) ndiye aliibuka mshindi kwa kuwaacha wenzake na Nazi nyingi zaidi wakiendelea kuchuana wawili.

 Wasanii wa Kikundi cha Sanaa na michezo ya asili cha Luperwa Zanzibar Group, chenye maskani yake Bububu, wakitoa burudani wakati wa hafla ya kufunga Tamasha hilo, lililofungwa na Mhe. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, jana Juni 15, 2013 Mangapwani. 


 Wasanii wa Kikundi cha Sanaa na michezo ya asili cha Luperwa Zanzibar Group, chenye maskani yake Bububu, wakitoa burudani wakati wa hafla ya kufunga Tamasha hilo, lililofungwa na Mhe. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, jana Juni 15, 2013 Mangapwani. 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifunga mlango wa Kibanda cha Makuti kama ishala ya kufunga rasmi Tamasha hilo la Watu wa Mangapwani, jana Juni 15, 2013, lililofunguliwa na Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein, Juni 14.  

KAMPUNI YA STEPS YANOGESHA TUZO ZA BONGO MOVIE



Mkurugenzi wa Kampuni ya Steps, Diresh Solanki akimpa tuzo msanii bora wa kiume katika tasnia ya filamu nchini Jacob Stevin JB wakati wa utoaji wa tuzo hizo zilizofanyika usiku wa kuamkia leo na kuhudguliwa na wasanii wengi nchini hii ni kwa mara ya kwanza steps inaandaa tuzo hizi zitakazokuwa zikitolewa kila mwaka.Picha nawww.burudan.blogspot.com
Pazia ra Tuzo za Steps Bongo Movie Awards ukiwa umefunguliwa na waziri wa Sayansi na Teknolojia Makame Mbawala

Mzee Majuto akipokea Tuzo ya msanii bora wa uchekeshaji


Msanii Stiv Nyerere akipokea Tuzo

Msanii Nice Mohamedi 'Mtunis' akipokea tuzo ya Mwaka 2012 zilizoandaliwa kwa mara ya kwanza na kampuni ya Steps Entatainment tuzo hizi zitakazokuwa zikitolewa kila mwaka.Picha na www.burudan.blogspot.com

MAMA SHILOLE AKIWA JUKWAANI

Mtoto Jenifa akichukua tuzo yake

Add caption

Msanii Niva akichukua TUZO ya msanii bora Chipkizi kulia yupo msanii mwenzake Rado

Photo: Mjumbe wa Kamati ya saidia Taifa Stars Ishinde, Ridhiwani Kikwete kushoto akimkabidhi tuzo Haji Adamu kwa niaba ya Jimmy Mponda aliyeshinda msanii bora wa Filamu za Mapigano wakati wa utoaji wa tuzo hizo zilizofanyika kwa mara ya kwanza nchini na kuandalia na kampuni ya Steps Picha na www.burudan.blogspot.com
Mjumbe wa Kamati ya saidia Taifa Stars Ishinde, Ridhiwani Kikwete kushoto akimkabidhi tuzo Haji Adamu kwa niaba ya Jimmy Mponda aliyeshinda msanii bora wa Filamu za Mapigano wakati wa utoaji wa tuzo hizo zilizofanyika kwa mara ya kwanza nchini na kuandalia na kampuni ya Steps Picha na www.burudan.blogspot.com

Mjumbe wa Kamati ya saidia Taifa Stars Ishinde, Ridhiwani Kikwete wa tatu kushoto akiwapongeza baadhi ya wasanii wa marehemu Kanumba baada ya kuwakabizi tuzo






Mkurugenzi wa Kampuni ya Steps Dilesh Solanki akimkabizi tuzo ya mwongozaji bora wa filamu nchini kwa mwaka 2012 Vicent Kigosi 'Ray ' wakati wa utoaji wa tuzo hizo zilizofanyika usiku wa kuamkia leo na kuhudguliwa na wasanii wengi nchini hii ni kwa mara ya kwanza steps inaandaa tuzo hizi zitakazokuwa zikitolewa kila mwaka.Picha nawww.burudan.blogspot.com

Mkurugenzi wa Kampuni ya Steps Dilesh Solanki akifafanua jambo baada ya kumkabizi tuzo Vicent Kigos 'Ray' ya mwogozaji bora wa filamu nchini kwa mwaka 2012 wakati wa utoaji wa tuzo hizo zilizofanyika usiku wa kuamkia leo na kuhudguliwa na wasanii wengi nchini hii ni kwa mara ya kwanza steps inaandaa tuzo hizi zitakazokuwa zikitolewa kila mwaka.Picha na www.burudan.blogspot.com

Wafanyakazi wa Kampuni ya Steps wakipokea tuzo

Baazi ya wasanii wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukabiziwa tuzo zao za kwanza kwa mwaka 2012 zilizozaminiwa na kampuni ya steps Picha nawww.burudan.blogspot.com

MPIGA PICHA mOHAMED aralakia  ZA KAVA MBALIMBALI ZA KAMPUNI YA STEPS AKIPOKEA TUZO

:KAMPUNI ya Usambazaji wa filamu ya Steps Entatainment ya jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki iliyopita ilitoa tuzo kwa wasanii bora waliofanya vizuri katika tasnia ya filamu nchini kwa mwaka 2012 ikiwa ni kwa mara ya kwanza kuanzishwa kwa tuzo hizo

Akizungumzia tuzo hizo Mkurugenzi wa Kampunu hiyo Direshi Solanki amesema kuwa tuzo hizo watakuwa wakizitoa kila mwaka kwa kuleta maendeleo ya filamu nchini kampuni hiyo iliyojikita katika kusambaza filamu za wasanii wameweka historia ya kuigwa kutokana na kuanzisha tuzo hizo

Baadhi ya washindi ambao walipatikana katika tuzo hizo wa kwanza ni Stevin Mangele 'Stive Nyerere', Issa Mussa 'Cloud 112' Mohamed Nurdini 'Chek budi' Nice Mohamed 'Mtunisi' Irene Paul akinyakuwa msanii bora chipkizi wa kike.
Wakati katika kinyanganyiro cha kumpata msanii bora wa kiume alinyakuwa Jacob Stevin 'JB' huku msanii bora wa kike ikienda kwa mwana dada Irene Uwoya na msanii bora wa filamu za mapingano ilikwenda moja kwa moja kwa Jimmy Mponda 'Jimmy Masta'

Wakati katika kipengere cha muongozaji bora wa filamu kilikwenda kwa vicent Kigosi' Ray' na kampuni yake ya RJ Filamu

Mbali na hivyo kulikuwa na tuzo za heshima kwa wasanii waliofanya vizuri rakini kwa sasa awapo duniani moja ni kwa Steven Kanumba,Juma Kilowoko 'Sajuki' John Stefano Maganga na 
Hussein Ramadhani Mkiety,'Sharo Milionea'

Katika utoaji wa tuzo huzo kulikua na burudani nyingi zikiongozwa na Odama Bendi

RAIS JK KUSHUHUDIA MTANANGE WA WABUNGE v WAKUU WA WILAYA ITAKAYOPIGWA UWANJA WA TAIFA JUNI 29

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mechi ya hisani itakayowakutanisha waheshimiwa wabunge na Wakuu wa wilaya, itakayopigwa Juni 29, katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Mechi hiyo itatanguliwa na ile ya Juni 22 mjini Dodoma, ambapo huko mgeni rasmi atakuwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ambapo lengo la mechi hizo ni kuchangisha fedha za ujenzi wa shule ya albino, huku kukipangwa kuwa na burudani za kila aina, sambamba na wasanii watakaoamua kuungana na serikali juu ya uchangiaji huo.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Msemaji Mkuu wa timu hiyo ya wakuu wa wilaya, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu, alisema kuwa huku mheshimiwa rais akiwa mgeni rasmi, ila wamejipanga imara kwa ajili ya kuwaonyesha kazi wabunge, ambao baadhi yao wameanza kujigamba dhidi ya mechi hiyo ya aina yake.
Alisema kuwa Watanzania wote watakaopata fursa ya kuhudhuria kwenye mechi hizo wataaburudika kwa kiasi kikubwa, huku wakiamini kuwa licha ya wakuu wa wilaya wengi kuwa mikoani, ila wana nguvu na ari ya kushinda mbele ya wabunge.
“Tupo imara na tutaanza mazoezi yetu kesho Jumatatu kwa kukutanisha wakuu wa wilaya wote waliokuwa kwenye timu hii, huku barua za kuwaombea mialiko kutoka kwa Wakuu wa Mikoa tayari zimeshafika kwa ajili ya kufanikisha zoezi hili.
“Katika mechi hizi, mwamuzi wa kati atakuwa atakuwa Reginald Mengi, ambaye ni Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, huku waamuzi wa pembeni wakiwa ni IGP Said Mwema na Stephen Wassira, ambapo wote watashiriki katika mchezo huu,” alisema.
Aliwataja Wakuu wa wilaya waliotwa kwenye uundwaji wa kikosi hicho kuwa ni pamoja na Venas Mwamoto (Kibondo), Ramadhan Maneno (Kigoma), Norman Sigara (Mbeya), Krispin Meela (Rungwe), Benson Mpesya (Kahama), Deodatus Kinanilo (Chunya), Herman Kapufyi (Same), Francis Isaac ( Chemba), Wilson Mkambaku (Kishapu), Yahya Nawanda (Iramba), Elibariki Kingu (Igunga), Festo Kiswaga (Nanyumbu), Paza Mwamlima (Mpanda), Abdallah Ulega (Kilwa), Seleman Mzee (Kwimba), John Mongela (Arusha), Konstantin Kanyasu (Ngara), Paulo Mzindakaya (Busega), Mrisho Gambo (Korogwe), uhingo rweyemamu handeni, Cristofa Magala( Newala), Erasto Sima (Bariadi), Jordan Rugimbana (Kinondoni), Joseph Mkirikiti (Songea), Ngemela Rubinga (Mpanda) nay eye mwenyewe anayotokea wwilaya ya Handeni, ambaye pia ni msemaji wa timu hiyo.
Aidha, Muhingo alitaja kikosi cha wanawake kuwa kinaongozwa na Beth Mkwasa (Bahi), Sarah Dumba (Njombe), Josephine Mapiro (Makete), Hafsa Mtasiwa (Pangani), Mboni Mgaza (Mkinga), Halima Dendegu (Tanga), Queen Mlozi (Singida), Angelina Mabula (Butiama), Merry Tesha (Ukerewe), Christina Mndeme (Hanang), Anna Magoha (Urambo) Jacqueline Liana ( Magu).

HAPPYNESS WATIMANYWA NDIE MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI

Mshindi wa taji la Redds Miss Kanda ya Kati Happiness Watimanywa (Katikati) akiwa na nyuso ya furaha mara baada ya kamati ya majaji kumtangaza mshindi katika kinyanganyiro kilichoshirikisha walimbwendwe 12 kutoka Mikoa ya Dodoma, Singida, Tabora na Kigoma Wa Kwa Kwanza kulia Ni Mshindi wa Tatu Jackline huku Mshindi wa Pili ni  ( Wa kwanza Kushoto) Sabrina Juma Kutoka Mkoani Tabora
Jaji Mkuu wa Shindano ya Kumsaka Mloimbwende wa Kanda ya Kati Mh Hashim Lundenga Akipungia mikono watanzania waliofika kushuhudia mlimbwende wa Kanda ya kati anapatikana
Mshiriki wa Kinyanganyiro Cha Redds Miss Kanda ya Kati Hawa Nyange akijitambulisha
 Mmoja wa Washiriki wa Kinyanganyiro Cha Kumtafuta Mlimbwende wa Kanda ya kati akijitambulisha mbele ya hadhara
 Muda wa Kuonyesha Vipaji ukawadia
 Mavazi ya Ubunifu
 Walimbwende walioingia hatua Ya Tano Bora
 Wadau wa Miss Tabora wakifuatilia shindano kwa ukaribu kabisa
Mratibu na mwandaaji wa Redds Miss Kanda ya Kati akitoa Maneno huku pembeni yake ni Mgeni Rasmi (katikati) Mh John Komba akiwa na baadhi ya wabunge wenzake kutoka Zanzibar
Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya Amin akicheza na mmoja wa mashabiki wake ambaye alikua akiigiza kama Linah jana wakati wa shindano la kumtafuta Redds Miss Kanda ya Kati
Mmoja wa mashabiki wakimtunza Mwanamziki wa Kizazi kipya Amin wakati alipokuwa akitoa Burudani Jana katika Kinyanganyiro Cha Kumtafuta Mlimbwende wa Kanda ya Kati
Baadhi ya wadau waliojitokeza kwenye kushuhudia Shindano la Redds Miss Kanda ya Kati lililofanyika Usiku wa Kuamkia Leo Katika Ukumbi wa Kilimani Mkoani Dodoma.Picha Na Josephat Lukaza Wa Lukaza Blog